Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Mwanamke wa Thamani, Hajira Bitebo, amewahimiza wanawake kujishughulisha na shughuli za maendeleo na kufanya kazi kwa bidii badala ya kubweteka kukaa nyumbani bila kujituma.

Bitebo amesema mwanamke anapofanya kazi na kujitegemea kiuchumi huweza kusaidia familia na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho, Blandina Lukindo, amewataka wanawake kujithamini, kujipenda na kujitambua ili kuimarisha nafasi yao katika jamii na kujenga maisha bora kwa familia na taifa kwa ujumla.

Lukindo amesema ni muhimu kwa mwanamke kujithamini na kujipenda kwani hatua hiyo humjengea kujiamini na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Baadhi ya wanawake waliohudhuria mkutano huo wamesema elimu waliyoipata imewapa hamasa ya kujitambua zaidi, kujipenda na kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha maisha yao









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...