Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 11, 2026 ameongoza Kikao cha kujadili Mapendekezo ya kufanya Maboresho ya Sheria ya Mapato ya baadhi ya Mifuko kilichofanyika kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Machi 11, 2026.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika Kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi.

Wengine ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wanu Hafidh Ameir, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonaz na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El - maamry.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...