Na Janeth Raphael- MichuziTv -Dodoma .
Serikali imetangaza mpango wa kuanzisha utafiti maalum utakaoweka msingi wa uanzishwaji wa Benki ya Vijana, hatua inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa vijana na kuondoa changamoto zinazowakabili katika kupata mikopo na mitaji ya biashara.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu, wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana kwa mwaka wa fedha 2026/27, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia vijana, Mhe. Joel Nanauka, amesema utafiti huo utaanza rasmi katika mwaka huo wa fedha.
Amesema lengo kuu ni kubaini muundo sahihi wa taasisi hiyo ya kifedha ambayo itakuwa maalum kwa vijana, ili kuhakikisha inazingatia mazingira yao, uwezo wao wa kiuchumi na mahitaji halisi ya soko la ajira na uwekezaji.
Kwa mujibu wa Waziri Nanauka, Benki ya Vijana itakuwa chombo cha kimkakati kitakachosaidia kukuza ubunifu katika huduma za kifedha, kuongeza fursa za uwekezaji kwa vijana na kuchochea ajira mpya nchini. Pia, itasaidia kujenga mfumo imara wa kifedha unaojumuisha makundi yote ya vijana bila vikwazo vya kimtaji.
Aidha, serikali imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha programu za mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana, sambamba na kuongeza upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema serikali pia inapanga kufanya utafiti wa kuanzisha Vituo vya Ubunifu kwa Vijana (Youth Innovation Hubs) vitakavyolenga kukuza vipaji, ubunifu na mawazo ya kibiashara. Vituo hivyo vitakuwa kiunganishi kati ya vijana na masoko, teknolojia pamoja na mitaji.
Pia, serikali itakuja na mfumo wa kitaifa wa kuratibu masuala ya maendeleo ya vijana pamoja na kuanzisha kanzidata ya taifa itakayokusanya taarifa muhimu za vijana ili kusaidia kupanga na kutekeleza sera kwa ufanisi zaidi.
Vilevile, mapitio ya sheria ya Baraza la Vijana yanatarajiwa kufanyika ili kuliboresha zaidi katika kusimamia na kuwakilisha maslahi ya vijana nchini.
Serikali imeeleza kuwa hatua hizi zote zinalenga kuongeza ushiriki wa vijana katika uchumi na kuhakikisha wanakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa kupitia mfumo jumuishi wa kiuchumi na kijamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...