Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imepokea vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa kimaabara kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), ikiwa ni pongezi  baada ya kutambua mafanikio yaliyofikiwa na  Tanzania  katika udhibiti wa dawa za kulevya nchini.

Pongezi hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na ujumbe wa UNODC ukiongozwa na Mwakilishi wa  Kanda ya Afrika Mashariki, Ali El-Bereir, ambaye aliipongeza Tanzania kwa jitihada zinazofanyika katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu.

Vifaa hivyo  hutokewa mahsusi kuzijengea uwezo taasisi zinazosimamia udhibiti wa dawa za kulevya katika ngazi ya kimataifa chini ya mpango wa Kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP). huo umetolewa chini ya mpango wa kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP) 

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine za kisasa zenye uwezo wa kubaini kwa haraka aina mbalimbali za dawa za kulevya na kemikali zinazodhibitiwa hata zikiwa ndani ya vifungashio vyake bila kufunguliwa. Hivyo, kuwezesha ufanisi wa kichunguzi na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka. 

Aidha, UNODC imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo maafisa  wa DCEA Ili kuimarisha mapambano. 







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...