Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia Masuala ya Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.
Makamu wa Rais amewapongeza viongozi na wataalamu wote walioshiriki katika kikao hicho kwa jitihada walizofanya wakati wa maandalizi na majadiliano.
Katika kikao hicho Hoja ya Uingizaji wa Sukari kutoka Zanzibar katika Soko la Tanzania Bara imeridhiwa na kuondolewa katika orodha ya Hoja za Muungano, ambapo imeshuhudiwa kusainiwa kwa Hati ya makubaliano ya kuondoa Hoja hiyo katika orodha ya Hoja za Muungano ambayo ni miongoni mwa hoja nne za Muungano zilizokuwa zimesalia.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili ya Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma,Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Kiongozi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Saleh Juma Mussa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi pamoja na Wataalamu mbalimbali.
















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...