Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenan Kihongosi amesema siasa ni hesabu na wao wamekuwa wakishinda siku zote kwa sababu ya idadi kubwa ya wanachama walionayo.

Kihongosi ameeleza hayo leo Aprili 16,2026 alipotembelea na kuzungumza na wananchi na wanachama wa shina namba 12 Tawi la Bugulula Kata ya Bugulula wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza hayo Kihongosi amesema ukiangalia idadi kubwa ya watu waliopo hapo katika Shina namba 12 ni 200 kwa kudaria na Wilaya hiyo ina jumla ya mshina 3,614 na kuzidisha na idadi ya shina hilo moja unapata idadi kubwa ya watu.

“Ukiangalia idadi ya watu hapa, wanakadiriwa kuwa kama mia mbili katika shina moja, ukizidisha kwa mashina yote, unapata idadi kubwa sana ya watu, alafu kuna mtu anauliza sisi tutashindaje? Mwambie tunashinda kwa sababu tuna watu hawa ndio msingi wetu. 

Ameongeza; “Siasa ni hesabu, vyama vingine vinawezaje kushinda kama havina watu, anashinda vipi bila idadi hii haiwezekani. Sisi tunaenda kwa namba, tunaenda kwa hesabu”.

Amesema hiyo  ndiyo nguvu ya CCM kama chama  wanaisimamia serikali kuhakikisha miradi inatekelezwa. wanakagua, wanaripoti kwa viongozi wa juu, na kama mambo ni mazuri yanaonekana, kama ni mabaya, wananchi wanafahamu.

Amesiaitiza tofauti na vyama vingine ni kwamba  vinawahamasisha watu kupigana na kufanya vurugu, lakini  watu wa Bugulula wanachotaka ni maendeleo wanahitaji barabara, umeme, shule, hospitali na pembejeo za kilimo, kwani hayo ndiyo mambo ya msingi.

“Lakini Mtu anakuja anasema kamanda, pambana, zungusha Wewe unapigana na nani? Msijidanganye,  hakuna faida ya vurugu mimi nasema watu waandamane kutafuta pesa hayo ndiyo maandamano mazuri baba ukirudi nyumbani na hela, chakula au mazao, familia yako inanufaika,” amesema Kihongosi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...