Pamela Mollel Arusha 

MAWAKALA WA BIMA wametakiwa kuzingatia  uadilifu, pamoja na kujenga mahusiano imara na wateja, pamoja na kuendelea kujifunza ili kuendana na mabadiliko ya soko.

Hayo yamesemwa  jijini Arusha na  Meneja wa Bima kanda ya kaskazini (TIRA) Dokta  Emmanuel Lupilya wakati akizungumza kwenye kikao maalumu kilichowakutanisha mawakala wa bima kutoka jijini Arusha .

Dokta Lupilya amesema lengo la kikao hicho ni kujadili na kuweza kuboresha maswala mbalimbali ya bima pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Dokta Lupilya amesema kuwa,Wakala wa bima wametambuliwa kwa mchango wao mkubwa katika kulinda maisha na mali za Watanzania .

Dokta Lupilya amesema kuwa,kusanyiko hilo limewaleta kutambua mchango mkubwa hasa kwa mawakala wanaofanya kwa ajili ya  nchi yetu  .

"Ni dhahiri kuwa wanaendesha biashara hizi kwa kuzingatia weledi kwa  kuthamini utu wa wananchi pamoja na udhubutu wao katika kuhakikisha wanalinda ndoto za watanzania ."amesema .

Ameongeza  kuwa, mafanikio  yao wanayofanya yasihesabiwe tu katika mikataba wanayoandika bali ihesabiwe katika watu wangapi wamewahubiria habari za bima watu wangapi wamewasaidia katika maswala yao pamoja na familia walizosaidia katika kuingia kwenye mfumo mzima wa bima .

"Kwa kufanya hivyo watakuwa wamehesabiwe ile thamani yao kwa kuelimisha jamii na imani waliyoonyesha kwa jamii kuwa bima sasa sio kitu cha anasa bali  ni kitu cha muhimu na kila mwananchi lazima awe nacho ."amesema Dokta Lupilya. 

"Swala la kutoa huduma z bima sio swala dogo ni swala zito na ni swala ambalo linahitaji weledi zaidi na mawakala hawa wamekuwa mfano wa kuigwa kwani wamekuwa lango la kuwezesha uelewa wa maswala la bima kwa  jamii."amesema .

"Kilio changu mimi ni kuhakikisha kuwa kukua kwa sekta ya bima kuna mchangao mkubwa sana wa mawakala  kuwezesha sekta kukua na mawakal hao wanafanya kazi kubwa ."amesema  Dokta Lupilya. 

 Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mawakala wanakuwa na wao kama  mamlaka ni kuhakikisha wanawawekea mazingira rafiki ambayo yatawawezesha kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa .

Aidha amewataka pia mawakala kufanyiwa mafunzo mara kwa mara katika maswala ya fedha ili wajue namna ya kutunza kile wanachokipata .

Aidha ametoa kwa makampuni kuonyesha mfano kwa maana ya kupeleka mafunzo ya maswala ya mahesabu ili wajue namna ya kuweza kukua na kuweza kujifunza teknolojia mpya kwani kuna wakati wataanza kuuza bidhaa zao kupitia teknolojia kwan8 teknolojia inauza zaidi .

"Tuwafundishe hawa namna ya kutumia teknolojia kwenye biashra ya bima na kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana ."amesema Dokta Lupilya. 

Nao Baadhi ya mawakala wakizungumza kwenye kikamo hicho , wamesema kuwa ,malalamiko makubwa wanayolalamikia.ni swala la mzigo mkubwa ambao mawakala wanayabeba jambo ambalo mawakala wengi wanashindwa kuendesha hiyo biashara kutokana na changamoto hizo kwani soko limekuwa na ushindani mkubwa na gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa kwani mabenki yameingia ambapo ameomba mamlaka hiyo iangalie namna ya kuwabeba mawakala na mawakala ndo wenye biashara ya moja kwa moja .

"Tunachoomba mhakikishe mnawabeba hawa mawakala kwani mzigo ni mkubwa sana na hawawezi na mjitahidi  kuwawezesha mawakala na muwape  motisha pia ."amesema .







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...