Na John Mapepele, New York -Marekani
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameongoza timu ya Tanzania katika Mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Idadi ya Watu na Maendeleo unaofanyika New York Nchini Marekani.
Mhe. Mchengerwa amesema Mkutano huo ambao umeanza leo Aprili 13,2026 na utaendelea hadi Aprili 17, 2026 unalenga kuimarisha uhusiano kati ya idadi ya watu, teknolojia, utafiti na maendeleo endelevu, pamoja na kusaidia nchi kupanga sera bora za maendeleo kulingana na takwimu na ubunifu wa kiteknolojia.
Mhe.Mchengerwa amefafanua kuwa mambo mengine muhimu yatakayojadiliwa wakati wa vikao hivyo ni pamoja na Teknolojia katika afya ya uzazi na afya ya jamii ikiwemo teknolojia mpya za uzazi wa mpango (contraception), Utafiti katika "reproductive health", matumizi ya "telemedicine na digital health platforms" pamoja na upatikanaji wa huduma za afya kwa vijana na wanawake.
Aidha, Mhe. Mchengerwa ambaye pia ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia eneo la Madawa na Vifaa Tiba, Bwana Emmanauel Tayari anayetarajia kutoa mada mahususi kwenye mkutano huo kuhusu Tanzania.
Sanjari na vikao hivyo, Mhe. Mchengerwa anatarajia pia kuwa na vikao kadhaa na wakuu mbalimbali wa mashirika ya Afya, na mabalozi wa nchi mbalimbali kuzungumzia masuala mbalimbali ya kimkakati katika sekta ya Afya.
Mkutano huu unahusisha zaidi ya nchi 193 kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na mashiriki yote makubwa yanayojishuhulisha na masuala ya afya.



.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...