Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dk. John Mduma, amesema hivi karibuni mfuko huo unatarajia kuzindua lango la huduma binafsi kwa mfanyakazi na ‘Appliction’ maalumu ya simu inayojulikana kama WCF Mkononi.
Dk. Mduma ametoa kauli hiyo leo Aprili 16, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Mkutano Maalumu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioitishwa kwa lengo la kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya jukwaa hilo.
Akielezea kuhusu mfuko huko Dk. Mduma amesema kuhakikisha utekelezaji thabiti wa majukumu na utoaji wa huduma, Mfuko umewekeza kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya TEHAMA.
“Hadi sasa zaidi ya asilimia 95 ya huduma zote tunazozitoa zinapatikana kwa Online kuanzia kusajili wanachama, ukusanyaji wa michango, uwasilishaji na uchakataji wa madai hadi malipo ya fidia. Mafanikio haya yametuwezesha kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.
“Katika utekelezaji wa kazi zetu tumekuwa tukikutana na maswali kutoka kwa wafanyakazi wengi wakitaka kujua kama wanachangiwa na waajiri wao au hapana.
“Hii inatokana na ukweli kwamba, tofauti na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii, kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi anayepaswa kuchangia ni mwajiri ambaye anatakiwa kuwasilisha WCF asilimia 0.5 ya mshahara wa kila mfanyakazi wake; na ndio maana hata mkiangalia katika zile ‘salary slips’ zenu hamuoni michango iliyopelekwa WCF.” amesema.
Dk. Mduma amesisitiza katika kutatua changamoto hiyo wameamua kuja na lango la Hlhuduma binafsi kwa Mlmfanyakazi na ‘Appliction’ (maombi) maalum ya simu inayojulikana kama WCF Mkononi ambayo tutaizindua hivi karibuni.
Kupitia mfuko huo Mfanyakazi utaweza kupata huduma za kuboresha taarifa zake binafsi, kuangalia l taarifa ya michango yake inavyowasilishwa na mwajiri wake WCF,kufuatilia madai yake ya fidia.
Pia, kuona na kupakua barua mbalimbali kutoka WCF, Kuwasiliana moja kwa moja na WCF na Kuwasilisha maoni.
Dk. Mduma amesema wanaamini matumizi ya Mifumo hiyo yatakapoanza hivi karibuni, wafanyakazi wataweza kufahamu michango yao ya kila mwezi na kusaidia kufuatilia kwa waajiri wao kuhusu utekelezaji wa takwa hilo la kisheria.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...