Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi, ametembelea kituo cha uwekezaji cha NBAA "APC Hotel and Conference Centre" kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa kituo hicho kwa lengo la kujionea utendaji kazi.

Katika ziara hiyo ya kikazi, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho, akiwahimiza kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na kujituma ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja na wageni wanaotumia kituo hicho kwa kazi mbalimbali. Pia alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho ili kujionea hali halisi ya utoaji huduma na miundombinu iliyopo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi, akibainisha kuwa mafanikio ya taasisi yoyote yanategemea mshikamano na uwajibikaji wa kila mfanyakazi.

“Ni muhimu kila mmoja wetu akatimiza wajibu wake kwa ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya kazi, ili kuendelea kujenga taswira nzuri ya Taasisi na kuvutia wateja zaidi,” alisema CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi.

Aidha, alibainisha kuwa "APC Hotel and Conference Centre" ni moja ya vitega uchumi muhimu vinavyochangia mapato ya Taasisi, hivyo ni lazima ihudumie kwa kiwango cha juu kinachokidhi mahitaji ya soko la ushindani.

Naye Meneja wa Kituo hicho cha Uwekezaji CPA Wenceslaus Mkenganyi, alimshukuru CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi kwa ziara hiyo, akisema imewapa hamasa kubwa wafanyakazi na kumhakikishia kuwa wataendelea kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za uongozi mpya wa NBAA za kutembelea na kujifunza utendaji kazi wa Taasisi na vitega uchumi vyake, pamoja na kusikiliza changamoto na maoni ya wafanyakazi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Uwekezaji cha APC mara baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utoaji huduma na miundombinu iliyopo.
Meneja wa kituo cha Uwekezaji cha APC, CPA Wenceslaus Mkenganyi akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi kuzungumza na wafanyakazi alipotembelea kituo hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Uwekezaji cha APC wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi akitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha Uwekezaji cha NBAA "APC Hotel and Conference Centre"  kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya utoaji huduma na miundombinu iliyopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...