Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Katika hotuba yake ya mapito na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2026/27 iliyowasilishwa leo Bungeni, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesisitiza juhudi za Serikali za kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu unasaidia ukuaji wa kiuchumi na kijamii nchini.
Dkt. Nchemba ameeleza kuwa nishati ya umeme ni kichocheo kikubwa cha maendeleo, hasa katika viwanda, teknolojia na matumizi ya nyumbani. Kutokana na mikakati ya Serikali, miradi mbalimbali ya uzalishaji wa umeme, ikiwemo ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere kwa kutumia fedha za ndani, imekamilika na sasa nchi ina ziada ya umeme.

Aidha, Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa umeme ili kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme na kuunganisha wilaya ambazo hazipo kwenye gridi ya Taifa.
Waziri Mkuu ameelekeza Wizara ya Nishati kuhakikisha upatikanaji wa umeme katika vitongoji, hospitali, vituo vya afya, zahanati, shule, taasisi za dini na visima vya maji. Vilevile, amesisitiza ushirikiano na Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa mradi wa Gridi Imara zinatolewa kwa wakati ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme.
Mbali na umeme, Serikali imeongeza matumizi ya gesi asilia, ambapo kutoka Julai 2025 hadi Februari 2026, mtandao wa usambazaji wa gesi umeongezeka kutoka kilomita 184.8 mwaka 2024/25 hadi kilomita 243.6. Vituo 14 vya kujaza gesi asilia vilivyokamilika vinatoa huduma kwa viwanda, taasisi na nyumbani.
Dkt. Nchemba pia ameeleza kuwa licha ya changamoto za kiusalama kikanda na kimataifa, Serikali inaendelea kusimamia upatikanaji wa bidhaa za mafuta na kuhakikisha bei zao zinabaki himilivu.

Serikali pia inaendeleza miradi ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta, ikiwemo ghala lenye uwezo wa kupokea tani 308,110 katika Bandari ya Dar es Salaam, ambalo sasa limefikia asilimia 30 ya ujenzi, na kuongeza uwezo wa Bandari ya Mtwara kutoka tani 29,280 hadi tani 110,221.
-Kwa mwaka 2026/2027, Serikali itazingatia:
Kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kukidhi mahitaji ya nishati.
Kusambaza umeme katika vitongoji ambavyo havijapatiwa huduma.
Kuendeleza shughuli za kutafuta, kusafirisha, kuhifadhi na kusambaza mafuta na gesi asilia.
Kukamilisha mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika taasisi.
Kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.
Hata hivyo Dkt.WIGULU amesema kuwa jitihada hizo za Serikali zinalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za nishati na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...