Na Byera  Deus,Bukoba,

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya elimu na Afya  vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 103.2 kwa shule za msingi ,sekondari  na zahanati mkoani Kagera  huku wakifuta simanzi kwa kutoa Viti mwendo 30 kwa watoto wenye ulemavu Mgeza Mseto 

Msaada huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima Hafla ambayo imefanyika katika shule ya msingi Mgeza mseto nakugusa vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu ,kupokea viti mwendo huku Halmashauri za Bukoba,Manispaa y Bukoba,Muleba na Missenyi nao wakinufaika na  msaada ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, 

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya NMB, Meneja wa Kanda ya Ziwa  Faraja Ng'ingo amesema benki hiyo inaendelea kujikita katika kusaidia jamii, akibainisha kuwa hadi sasa NMB ina wateja zaidi ya milioni 8, huku tangu mwaka 2021 ikiwa imerejesha kwa jamii zaidi ya shilingi Bilioni  24 katika miradi mbalimbali bara na visiwani na Kila mwaka utenga asilimia 1 ya faida kurejesha kwenye jamii.

Alisema msaada huo unalenga kupunguza changamoto za vifaa mashuleni na kuboresha huduma za afya katika zahanati  vitu ambayo jamii inavitumia Kila siku 

Vifaaa vilivyotolea ni viti Mwendo,Madawati ,vitanda vya mabweni ,mashuka,vifaaa vya kuezekea zahanati samani mbalimbali kwa Magereza 

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,  Erasto Sima, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, amesema vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa na vitasaidia kupunguza changamoto za wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo kutokana na uhaba wa vifaa.

 Aidha, amewahimiza wadau na wananchi wengine kuiga mfano huo kwa kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu hata katika matukio binafsi kama sherehe za kuzaliwa.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Mheshimiwa Acton Rwankomezi, ameishukuru NMB kwa mchango huo, akieleza kuwa bado manispaa inakabiliwa na upungufu wa zaidi ya madawati 1,000na kudai kuwa  msaada uliotolewa, ukiwemo wa madawati, utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa Cha  changamoto hiyo. 

Nao walimu pamoja na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu wamepongeza msaada huo na kuitaka jamii kuendelea kushirikiana kusaidia kundi hilo muhimu ,hasa wanafunzi wa Mgeza Mseto wenye ulemavu ambao wanakabiliwa na mahitaji maaalumu.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...