Timu ya Mchezo wa kuvuta kamba ya Wanaume na wanawake ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeiburuza bila huruma timu pinzani za Utamaduni na Mashtaka 2-0 katika michezo ya Mei Mosi iliyoanza kurindima Mkoani Njombe.
Akizungumza baada ya michuano hiyo, Mwenyekiti wa Maliasili Sports Club Bw. Elia Mutalemwa amesema kuwa, siri ya ushindi huo ni maandalizi mazuri chini ya uangalizi wa viongozi wa Wizara.
Kocha wa timu hiyo Bw. Gabriel Michael amefafanua kuwa ushindi wa 2-0 wa timu ya Maliasili Wanawake Kamba dhidi ya timu ya Utamaduni, ulikuwa mwepesi kwao kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwa wachezaji wake.
Amewashukuru wakazi wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao jambo lililo inua ari kubwa kwa wachezaji na kuipelekea pia timu ya Maliasili Wanaume kuiburaza bila huruma 2-0 timu ya Mashtaka na kuifanya iondoke uwanjani kwa majonzi makubwa.
Naye Bi. Neema Mkinga mkazi wa Makambako amesema amevutiwa na Michezo hiyo hasa namna timu zilivyojipanga hususan timu za Maliasili na Utalii.



.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...