Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuboresha upatikanaji wa dawa na bidhaa za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma nchini, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya ugavi ili kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati na kwa ubora unaokidhi viwango.
Amesema hayo Aprili 2, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya afya kilichofanyika katika Bohari ya Dawa (MSD), Keko, ambapo alibainisha kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali umeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa na kufikia viwango vinavyoridhisha.
“Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya usimamizi na ugavi ili kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati katika maeneo yote ya nchi. Maboresho haya yanachangia kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya afya,” amesema Mchengerwa.
Aidha, amesema Serikali imeelekeza juhudi katika kuhakikisha kunakuwepo uwiano sahihi kati ya mahitaji halisi na upatikanaji wa dawa, hatua inayosaidia kuongeza ufanisi na matumizi bora ya rasilimali zilizopo.
Katika kikao hicho, Mchengerwa alisisitiza pia umuhimu wa Bohari ya Dawa (MSD) kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi, manunuzi na usambazaji wa dawa ili kuepuka upungufu katika vituo vya kutolea huduma.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Serikali, Grace Magembe, amesema Serikali itaendelea kusimamia matumizi sahihi ya dawa pamoja na kuhakikisha upatikanaji wake katika ngazi zote za huduma za afya nchini.
Dkt. Magembe alisisitiza kuwa dawa si bidhaa ya kawaida bali ni kemikali yenye uwezo wa kutibu au kusababisha madhara iwapo haitatumika kwa usahihi, hivyo usambazaji wake lazima uzingatie uwepo wa wataalamu wenye ujuzi pamoja na miundombinu ya kumhudumia mgonjwa endapo atapata madhara.
Akijibu hoja za wananchi, alisema Serikali inatambua changamoto zilizopo, ikiwemo upatikanaji wa baadhi ya dawa katika zahanati na vituo vya afya, na kwamba hatua zinaendelea kuchukuliwa ili kuboresha hali hiyo.
Kuhusu upatikanaji wa dawa katika ngazi mbalimbali, alisema upangaji wake unazingatia tafiti za kisayansi na Orodha ya Dawa Muhimu (Essential Drug List), ambapo kila ngazi hupangiwa dawa kulingana na aina ya huduma na uwezo wa kituo husika.
Akizungumzia suala la dawa kuisha muda wake (expiries), Dkt. Magembe alisema hali hiyo ni ya kawaida duniani kote kutokana na muda wa matumizi wa dawa na mabadiliko ya kisayansi, na kusisitiza kuwa Serikali haiwezi kuruhusu matumizi ya dawa zisizo na ufanisi.
Alibainisha kuwa kiwango cha dawa zinazoisha muda wake nchini ni asilimia 1.2, chini ya kiwango kinachokubalika kimataifa cha asilimia tano, jambo linaloonesha usimamizi mzuri.
Aidha, alisema Serikali imeanza kushusha huduma za magonjwa adimu kama sickle cell hadi ngazi ya hospitali za wilaya na kuingiza dawa zake katika mfumo wa ununuzi ili kupunguza gharama kwa wananchi.
Dkt. Magembe pia aligusia matumizi ya majina ya dawa (brand names badala ya generic names), akisema Serikali itatoa maelekezo kurekebisha hali hiyo ili kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa dawa.
Aliongeza kuwa Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka takribani shilingi bilioni 30 hadi kufikia bilioni 398 mwaka 2025, hatua iliyosaidia kuongeza upatikanaji wa dawa hadi asilimia 88 kwa sasa.
“Tutajipanga zaidi kutoa elimu kwa wananchi waelewe sayansi ya dawa na matumizi yake, kwa sababu dawa si chakula; ni sumu isipotumika vizuri,” amesema Dkt. Magembe.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Seif Shekalaghe, amesema zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wanaokwenda hospitali hupatiwa dawa, huku wengine wakipewa ushauri wa mabadiliko ya mtindo wa maisha ikiwemo mazoezi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, amesema taasisi hiyo imeendelea kuboresha utendaji wake kwa kuimarisha mifumo ya kidijitali, kuongeza ufanisi katika manunuzi na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Ameeleza kuwa ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka shilingi bilioni 15.9 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 98 mwaka 2024/2025, huku lengo la mwaka huu likiwa kufikia kati ya bilioni 120 hadi 130.
Aidha, amesema utegemezi kwa wasambazaji wa nje umepungua kutoka asilimia 82 hadi asilimia 38, wakati ununuzi kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka hadi asilimia 75.
Alibainisha kuwa hatua hizo zimewezesha hata dawa ambazo awali zilikuwa ngumu kupatikana, ikiwemo za saratani, kupatikana kwa urahisi zaidi na kwa gharama nafuu.
Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora nchini.

Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wananchi mubashara kupitia mfumo ongea na Waziri kupitia namba ya 199, leo Aprili 2, 2026, wakati wa kikao kazi na wadau wa Afya kilichofanyika Bohari ya Dawa, jijini Dar es Salaam

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...