Na Diana Byera,Bukoba.


SERIKALI imetoa Sh. 16 kwa ajili ya kufanya maboresho ya upanuzi na njia za kusambaza umeme kwenye kituo cha kupokea,kupoza na kusambaza umeme cha Kibeta wilayani Bukoba mkoani Kagera.

Kituo hicho kinahudumia wilaya ya Bukoba,Missenyi na Muleba kwa lengo la kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Kagera

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera Mhandisi Tawakal Rwahila amesema mradi wa upanuzi wa kituo cha Kibeta umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Amefafanua kituo hicho kilijengwa mwaka 1993 kikiwa na uwezo wa megawati 20, lakini kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme kwa wananchi na shughuli za kiuchumi, Serikali ilianza rasmi mradi wa upanuzi mwaka 2023 kwa lengo la kuongeza uwezo hadi kufikia megawati 120.

Akieleza maendeleo ya mradi huo, Mhandisi Rwahila amesema tayari vifaa muhimu vimewasili na vinaendelea kufungwa, ikiwa ni pamoja na vivunja umeme (circuit breakers) vya kisasa, njia ya ziada ya usambazaji (feeder), pamoja na transfoma inayopunguza msongo wa umeme kutoka kilovolti 33 hadi kilovolti 11.

“Kwasasa majaribio ya awali ya mfumo yanaendelea, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukamilika kwa mradi huo kwa wakati uliopangwa.”

Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi TBEA kutoka nchini China, ambaye anaendelea na usimikaji wa miundombinu kwa viwango vinavyolenga kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya umeme katika mkoa wa Kagera.

Akieleza zaidi amesema kukamilika kwa kituo hicho kutaongeza uwezo wa usambazaji wa umeme pamoja na kupunguza changamoto ya ukatikaji wa umeme katika wilaya za Bukoba, Missenyi na Muleba huku akitaja kuwa hiyo ni Fursa ya kipekee kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika Fursa ya viwanda.

“Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, TANESCO imefanikiwa kusambaza umeme katika vijiji vyote 664 vya mkoa wa Kagera.Vitongoji 3,000 tayari vikiwa vimeunganishwa na huduma hiyo.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha umeme unafika hadi ngazi ya vitongoji, na mradi wa Kibeta ni sehemu muhimu ya kufanikisha azma hiyo.”







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...