Na. Josephine Majura, WF, Dodoma
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA), itaendelea kutathmini na kufuatilia kwa karibu ukuaji wa mapato ya kodi, ongezeko la idadi ya walipakodi na shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, ili pale vigezo vitakapokamilika hatua stahiki ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuipandisha hadhi kuwa mkoa wa kikodi.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Cecilia Paresso, aliyetaka kujua lini Serikali itaanzisha Mkoa wa Kikodi katika Wilaya ya Karatu.
Mhandisi Munde, alifafanua kuwa uanzishwaji wa mikoa ya kikodi hufanyika kwa kuzingatia vigezo vya kiutawala na kiuchumi ikiwemo kiasi cha mapato kinachokusanywa, idadi ya walipakodi, rasilimali zilizopo na mahitaji ya huduma katika eneo husika ili kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya kodi.
Aidha, alisema kuwa katika kuongeza ufanisi na kusogeza huduma kwa walipakodi, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilizipandisha hadhi baadhi ya wilaya za kikodi kuwa mikoa ya kikodi, ikiwemo Mkoa wa Kikodi wa Ilala, Kinondoni, Temeke, Kariakoo, Kahama, Tegeta na Pemba.
Mhandisi Munde, aliongeza kuwa Wilaya hizo zilizopewa hadhi ya mikoa ya kikodi zina wastani wa jumla ya walipakodi 906,399 (Ilala), 734,984 (Kinondoni), 563,568 (Temeke), 67,996 (Kariakoo), 82,054 (Kahama), 136,164 (Tegeta), na 28,076 (Pemba).
Kadhalika, katika mwaka wa fedha 2023/24 na 2024/25 wilaya hizo zilikuwa na wastani wa mapato ya kodi ya sh. bilioni 862.42 (Ilala), 574.36 (Kinondoni), 190.32 (Temeke), 136.03 (Kariakoo), 25.89 (Kahama), 101.1 (Tegeta), na 16.36 (Pemba).
“Kwa muundo wa kikodi wa sasa, Wilaya ya Karatu inatambulika kama wilaya ya kikodi chini ya mkoa wa kikodi wa Arusha ndani ya Idara ya Kodi za Ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)”, alisema Mhandisi Munde.
Wilaya ya Karatu ina jumla ya walipa kodi 4,672 ambao kwa kiasi kikubwa wanachangia ukusanyaji wa mapato ya kodi kutoka katika shughuli za utalii, madini na kilimo. Kadhalika, takwimu zinabainisha ukuaji wa asilimia 9.48 wa mapato ya kodi katika Wilaya hiyo, kwa kuzingatia makusanyo yenye jumla ya shilingi bilioni 10.07 kwa mwaka 2023/24 na sh. bilioni 11.12 kwa mwaka 2024/25.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Cecilia Paresso, aliyetaka kujua lini Serikali itaanzisha Mkoa wa Kikodi katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...