Na Mwandishi Wetu
WAFANYABIASHARA na mawakala wa zao la parachichi wilayani Rungwe wamepongeza juhudi za Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kwa kuendesha mchakato wa usajili unaolenga kuwatambua rasmi wadau wa sekta hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao wamesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuleta utaratibu mzuri wa biashara ya parachichi, hususan kwa kupunguza vitendo vya wizi na ulaghai vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu waliojiingiza kwenye biashara hiyo bila utambuzi rasmi.
Aidha, wameeleza kuwa kupitia usajili huo, itakuwa rahisi kwa mamlaka husika kufuatilia mwenendo wa biashara, kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara halali, pamoja na kuongeza uaminifu katika soko la zao hilo lenye mchango mkubwa kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Samwel Msuya, amewasisitiza wafanyabiashara na mawakala wa parachichi kuendelea kujisajili ili waweze kunufanya biashara katija utaratibu unaotambulika.
Amesema kuwa usajili huo si kwa wafanyabiashara na mawakala katika wilaya ya Rungwe pekee bali ni kwa mikoa yote inayizalisha parachichi nchini.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...