Katika jitihada za kuchochea matumizi ya simu janja na kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali, Yas imetambulisha promosheni ya muda mfupi katika kipindi hiki cha Pasaka inayotoa punguzo la bei kwa simu janja za ZTE.

Ofa hiyo ya siku tisa, imeanza rasmi tarehe 31 Machi na itadumu hadi tarehe 8 Aprili. Kupitia promo hiyo, malipo ya awali ya simu za ZTE yameshushwa kutoka Shilingi 45,000 hadi shilingi 25,000. Baada ya hapo, wateja wataendelea kulipia malipo nafuu ya kila siku ya shilingi 950 kwa kipindi cha miezi 12, hatua inayorahisisha zaidi umiliki wa simu janja kwa watanzania wengi.

Kama sehemu ya ofa hii, wateja pia watapata MB 150 za intaneti bure, zitakazowawezesha kuanza mara moja kufurahia mtandao mpana na wenye kasi zaidi nchini (Yas) pamoja na huduma zake za kidijitali.

Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja wa Vifaa, Mauzo na Usambazaji - Yas, Bi. Imelda Edward, alisema mpango huo unaakisi dhamira endelevu ya kampuni katika kupunguza pengo la kidijitali nchini.

“Promosheni hii ya Pasaka haihusu tu punguzo la bei. Inalenga kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuingia mtandaoni na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali. Kwa kutoa punguzo la bei kwenye malipo ya awali na kutambulisha mpango rahisi wa malipo ya kila siku, tunaondoa vikwazo vinavyowazuia Watanzania wengi kumiliki simu janja,” alisema.

Aliongeza kuwa promosheni hiyo inaendana na mkakati mpana wa Yas wa kutoa huduma bora na muunganisho wa kuaminika kote nchini.

“Tunajivunia kutoa mtandao uliotambuliwa kuwa wa kasi zaidi nchini Tanzania na Ookla kwa nyakati tatu mfululizo. Kupitia promosheni hii, tunataka kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea ubora wa mtandao wetu kupitia vifaa vya ZTE,” aliongeza.

Promosheni ya Pasaka inatarajiwa kuongeza matumizi ya simu janja, hasa kwa watumiaji wapya, huku ikiendelea kuchochea ukuaji wa mfumo wa kidijitali nchini. Wateja wanahimizwa kutembelea maduka ya Yas na mawakala walioidhinishwa kote nchini ili kunufaika na ofa hii ya muda mfupi kabla ya kumalizika.

Imelda Edward - Meneja wa Vifaa - Mauzo na Usambazaji - Yas Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...