
MECHI ya leo Uwanja wa Stamford Bridge inachezwa wakati Chelsea iko katika mtego mkubwa wa matokeo mabovu mfululizo, wakiwa wamepoteza michezo mitano ya Ligi Kuu bila hata kufunga bao hata moja .
Chelsea wamepoteza kwa mabao 0-1 dhidi ya Newcastle, 0-3 mbele ya Everton, na 0-1 nyumbani kwa Manchester United katika mechi za hivi karibuni, hivyo wanakabiliwa na shinikizo la kutaka kurejea kwenye ushindi mbele ya mashabiki wao .
Kwa upande mwingine, Nottingham Forest wana mwendo mzuri kabisa wakiwa hawajafungwa katika michezo mitano mfululizo ya ligi huku wakishinda Sunderland 5-0, Burnley 4-1, na Tottenham 3-0 ugenini, jambo linaloonyesha wana uhodari mkubwa wa kucheza ugenini . Nafasi ya Chelsea kwenye msimamo inawalazimu wakusanye pointi ili kuboresha hadhi yao,
Kocha wa mpito Chelesa Calum McFarlane anatarajiwa kuweka mbinu ili kuleta uthabiti baada ya lango lao kufungwa mara kwa mara mfululizo . Mbinu hii inamtegemea Liam Delap kuwa nguzo ya mbele wakati wachezaji pembeni wakijiunga naye kwa kasi, huku Enzo Fernández akiwa kiungo wa kupeleka mipira mbele .
Kwa upande wa Nottingham Forest, kocha Pereira Vitor anaweza kutumia na wachezaji pacha mbele kwa uwezo wa Chris Wood na Igor Jesus kuzichanganya beki za Chelsea.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Nguvu ya Forest ipo katika winga kama Morgan Gibbs-White na Omari Hutchinson ambao wanaweza kutumia nafasi za pembeni kumalizia mashambulizi, huku uwanja wa Stamford Bridge ukitarajiwa kuwa tayari kwa vita kubwa ya kiufundi.
Chelsea wanakosa nyota wao muhimu ambao wamekuwa nje kwa majeraha makubwa, wakiwemo Reece James aliyekaa zaidi ya mwezi mmoja na jeraha la paja lakini anaweza kurejea kwenye benchi, na Estevao aliyeumia na kuwa nje kwa msimu mzima. Levi Colwill anarudi kutoka jeraha lake lakini ana uwezekano wa kucheza mechi yake ya kwanza baada ya kupata dakika nzima kwenye timu ya vijana.
Forest watawakosa John Victor, Cunha, Murillo, Savona Nicolo, Hudson-Odoi Callum, Sangare Ibrahim, Ndoye Dan Liam Delap atakuwa mzigo wa Chelsea mbele ya lango, huku Chris Wood akiwa tishio kwa ulinzi wa Blue kwa uwezo wake wa kumalizia nafasi za mabao.
Katika historia ya makabiliano yao, Chelsea walishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Forest kwa mabao 3-0 ugenini Oktoba 2025 na 1-0 Mei 2025 huku Stamford Bridge wakitoa sare ya 1-1 Oktoba 2024 .
Chelsea wamekuwa na ubora katika michezo ya karibuni kati yao, wakiwa wameibuka na ushindi mara tano mfululizo katika michuano yote ikiwemo Kombe la FA . Hata hivyo, Forest wana rekodi nzuri uwanjani kwa Chelsea tangu wapande daraja, wakiwa na ushindi mmoja na sare mbili kwenye michezo hiyo. Jisajili


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...