Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi na watumishi wa sekta ya afya kuzingatia kutoa huduma za staha, utu na huruma kwa wananchi na kufuata maadili ya kada zao
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 3, 2026, jijini Mwanza wakati akifungua kikao kazi cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha miundombinu ya afya nchini, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mashine za kisasa kama MRI, CT-Scan na vifaa vya kusafisha figo pamoja na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma.
“Uwepo wa majengo mazuri na vifaa vya kisasa hauwezi kuwa na maana endapo huduma zinazotolewa hazina utu na huruma kwa wagonjwa,” amesema Mhe. Mchengerwa
Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa lugha chafu, rushwa, upendeleo na uzembe vinaweza kufuta kabisa thamani ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha sekta hiyo muhimu.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka watumishi kuhakikisha huduma zinatolewa kwa weledi, heshima na uadilifu, huku akionya kuwa, vitendo vya kuchelewesha huduma bila sababu, kudhalilisha wagonjwa au kuomba rushwa havitavumiliwa.
“Mgonjwa anapofika Hospitalini mara nyingi hubeba maumivu na hofu, hivyo namna anavyopokelewa inaweza kuwa sehemu ya tiba au kuongeza mateso zaidi,” amesisitiza
Ameongeza kuwa “Viongozi ndani ya Wizara ya Afya niwakumbushe kuwa uongozi bora hauhusiani na vitisho au ubabe, bali ni uwezo wa kusimamia, kuelekeza na kusahihisha kwa staha na heshima, malalamiko ya matumizi mabaya ya madaraka, unyanyasaji na udhalilishaji wa Watumishi wa ngazi za chini hii ni changamoto inayopaswa kushughulikiwa kwa umakini na kwa mujibu wa sheria,”
Mwisho, Waziri Mchengerwa ameleeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kusikiliza na kushughulikia malalamiko ili kuhakikisha Watumishi wote wanafanya kazi katika mazingira salama, yenye heshima na yanayolinda utu wao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...