-Yasisitiza inathamini maisha ya mtu na utu wa mtu kwani wananchi wana haki yakuishi bila hofu
-Pia yazungumzia inavyotambua nafasi ya vijana na hatua inazochukua kuwapatia fursa
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesemakinathamini maisha ya mtu na utu wa mtu , kwahiyo mambo ya utekaji ambayo yapoyanafahamika kwenye jamii na ukwelihaifurahishwi na matukio hayo.
Akizungumza katika mahojiano maalum naCrown Media yaliyokuwa yakiongozwa naMtangazaji Salim Kikeke, Chama hichokupitia Katibu Mkuu wake Dk.Asha-Rose Migiro kimeeleza hatua kwa hatua kuhusu matukio hayo ya utekaji.
“Chama Cha Mapinduzi kinasema nchi hii wananchi wake wana haki ya kuishi bilahofu,kwahiyo hatuwezi kuunga mkonosuala la utekaji.Tunaguswa sanakwasababu katika huu utekaji wako pia wanachama wetu wameathirika ,kwahiyohatuwezi kutoguswa.Wapo wanachamaambao nao wameingia katika kadhia hiyolabda sio wengi lakini na sisi ndani yaChama Cha Mapinduzi tunalifahamu hilo.
“Lakini tunafahamu vyombo vya dola nahasa Polisi wamekuwa wakifanyauchunguzi na sisi tunataka hatua kama hizozichukuliwe ili nchi yetu tuishi kwa utulivuna bila hofu.
Kuhusu ripoti ya Jaji Chande kuoneshamoja ya vichocheo vya vurugu za Oktoba29 ni vijana kutokuwa na fursa, kutokuwana nafasi za ajira, Dk.Migiro amesemawanapozungumzia vijana wanazungumziatnguvu kazi ya taifa hili ,pia wanazungumziamustakabali wa nchi yetu.
“Kwasababu kwa hakika taifa la leo na la kesho ni la vijana .Kwa kuzingatia hiloChama Cha Mapinduzi kimekuwa makinikatika Ilani yake.Tumebainisha umuhimuwa nguvu kazi ya vijana , tumebainishahaja ya kuwekeza na kuwa na mikakatikatika sekta mbalimbali, kilimo, viwanda , biashara ,uvuvi ,masuala ya kidijitali nakujenga weledi na stadi za maisha kwambatuwekeze zaidi hapa kwasababu yakuwajenga vijana wa taifa letu tukitambuanguvu ya taifa letu inatokana na nguvu yavijana,”amesema Dk.Migiro.
Pia amesema licha ya kuweka kwenye Ilani ,Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambayoilisimamiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweka wazi nafasi ya vijanana haja ya kuhakikisha wanachukua nafasiyao katika masuala yote ya kijamii, kiuchumi na kisiasa .”Kwahiyo vijana wanchi yetu hawajatelekezwa na Chama Cha Mapinduzi .
“Lakini mara baada ya Uchaguzi Mkuuwakati Rais anaunda Baraza la Mawazirialiunda wizara mahususi ya maendeleo yavijana na akaiweka chini ya ofisi yake ilijicho lakini liwe karibu kuhakikisha vijanaksauti yao inasikika katika mipango ya nchiyetu ,mchango wao unapatikana kwakutumia nguvu yao ,weledi wao nachangamoto zao zinatizamwa.
“Kuna mipango ya kuwawezesha kiuchumi,kuna mambo yamewekea mkakati ,eneo la mitaji na siku hizi vijana wanajiunga katikamakundi mbalimbali pamoja na uanzishwajiwa shughuli hasa za kiuchumi na kidijitali,hiyo yote ni mipango na sera za Chama Cha Mapinduzi. Hakuna namna CCM kitawaacha vijana wa nchi hii kwasababuhata takwimu za sensa zinaonesha vijanandio sehemu kubwa ya jamii yetu.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...