Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Endrew Kantimbo amesimamia zoezi la uundaji wa vikundi sita vya ulinzi shirikishi katika vijiji vya wakulima na wafugaji vilivyopo Kata ya Melela Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Hili limekuja Kufuatia kwa matukio mfululizo ya wizi wa mifugo katika eneo hilo ambapo wananchi hao wamesisitizwa kujilinda wenyewe kwa kushirikiana na Polisi kata wa eneo hilo.
Akizungumza na Wananchi hao katika eneo la Melela Kituoni Mei 3, 2026 Kamanda Kantimbo amesema viongozi wa vijiji na wananchi kwa ujumla wanapaswa kushirikiana na vikundi hivyo katika kuzuia uhalifu pamoja na kuwatolea taarifa wahalifu ili wadhibitiwe mapema.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Mvomero SSP Boniface Mwakalyegese amesema Wananchi watoe taarifa za uhalifu na kuacha kumaliza kesi kimila kwa kulipana Ng'ombe badala yake wafuate mnyororo wa sheria
Christopher Madukule mfugaji kwa niaba ya wananchi wenzake amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa Morogoro kupitia Kamanda wake kwa kitendo cha kutoka ofisini na katani kwaajili yao.
Naye, Sauda Kipira Mkulima wa eneo hilo amesema, mbali na kuzuia mifugo, Vikundi hivyo vinapaswa kuwadhibiti vijana wanaofanya matukuo ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wakike pindi wanapotumwa.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...