Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Peter Majule, ameibua mjadala bungeni kuhusu uwazi na haki katika biashara ya kaboni, akitaka serikali kueleza mikakati iliyopo kuhakikisha wananchi wa chini, hususan wanawake na vijana, wananufaika ipasavyo.

Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma, Dkt. Majule alitaka kujua ni viashiria gani na mfumo gani serikali imeweka kuhakikisha makisio ya mapato yanayotokana na misitu na ardhi ya wananchi yanazingatiwa kwa usahihi katika biashara hiyo inayohusisha wawekezaji.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Festo Dugange, alikiri kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa uwazi katika vipimo na malipo ya biashara ya kaboni kutokana na ushirikiano kati ya wadau mbalimbali.

Dugange alieleza kuwa serikali imeanza hatua za makusudi za kuboresha mfumo huo kupitia uanzishwaji wa kituo maalum cha kuratibu biashara ya kaboni kilichopo Morogoro, ambacho kinatarajiwa kuhamishiwa Dodoma.

Alisema kituo hicho kitashirikiana na wadau na serikali kuhakikisha vipimo sahihi vya kaboni vinapatikana na wananchi wananufaika moja kwa moja kulingana na kiwango halisi cha kaboni kinachozalishwa katika maeneo yao. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...