Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe umeadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Harare Zimbabwe.

Katika hafla hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, alipata fursa ya kumkaribisha Fredrick Shava, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Zimbabwe, aliyemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa, Prof. Amon Murwira, aliye mwakilisha mgeni rasmi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu isrmayo Miaka 62 Muungano amani umoja na Mshikamano ni Msingi wa Maendeleo endelevu, Balozi Kaganda alishukuru Serikali ya Zimbabwe, jumuiya za kidiplomasia na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao na Tanzania katika kukuza maendeleo huku akisisitiza kuwa Tanzania inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yameleta matokeo chanya.

Kwa upande wake, Waziri Shava aliipongeza Tanzania kwa kudumisha umoja na amani kwa miaka 62 ya Muungano, akieleza kuwa nchi hiyo imekuwa mfano bora katika ukanda wa SADC na Afrika kwa ujumla huku akibainisha kuwa Zimbabwe itaendelea kuthamini mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi na kudumisha ushirikiano wa maendeleo kati ya nchi hizo mbili.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...