Na Karama Kenyunko,Michuzi TV

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi wote nchini kwamba Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya wafanyakazi kadri uchumi utakavyoruhusu.

Dk.Samia ametoa ahadi hiyo leo Mei 1,2026 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja Lunyanywi mkoani Njombe.

“Wafanyakazi  ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo ya taifa. Hivyo niwahakikishie Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi pamoja na maslahi ya wafanyakazi nchini.”

Aidha amesema tayari Serikali imeanza kulipa madeni ya wafanyakazi ikiwemo malimbikizo ya mishahara, posho za likizo na uhamisho, huku akisisitiza madai yote yatapitiwa na kulipwa kwa haki huku akisisitiza kuboresha mazingira ya kazi yanaboreshwa na wafanyakazi wanapata haki zao.

Pia amesema kuna umuhimu wa kuwa na majadiliano ya pamoja mahali pa kazi ili kuimarisha mahusiano kati ya waajiri, wafanyakazi na Serikali.

Wakati huo huo Rais Dk.Samia  amesema kazi zenye staha ni msingi muhimu wa kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 ambapo amefafanua Tanzania inalenga kufikia uchumi wa dola za Marekani trilioni 1.52 ifikapo 2050.

Amefafanua kazi yenye staha inajengwa katika nguzo nne ambazo ni upatikanaji wa ajira, ulinzi wa haki kazini, hifadhi ya jamii na ushirikishwaji mahali pa kazi na kuongeza wafanyakazi ndiyo nguvu kazi ya taifa.

“Nitoe rai kwa Watanzania kuendelea kudumisha amani, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ili kulinda mafanikio ya taifa.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...