Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 500,000 kwa mwezi.

Rais Dkt. Mwinyi ametangaza ongezeko hilo la mshahara leo, tarehe 01 Mei 2026, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Dkt. Mwinyi amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutolewa kuanzia mwezi Januari 2027, na kufahamisha kuwa hatua hiyo imezingatia hali ya uchumi wa nchi, gharama za maisha, na kuwapatia motisha wafanyakazi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nane imepata mafanikio makubwa tangu ilipoingia madarakani mwaka 2020, kwa kufanikiwa kuimarisha maslahi ya wafanyakazi kupitia kurekebisha na kuongeza mishahara, kufanya mapitio ya posho na marupurupu ya watumishi, pamoja na kuimarisha mafao ya hifadhi ya jamii na kuanzisha mfuko wa bima ya afya kwa wafanyakazi wote pamoja na familia zao.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ametangaza kuwa Serikali imetenga nafasi za ajira 7,500 katika mwaka wa fedha 2026–2027, pamoja na kuendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...