
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi,
amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inatarajia kutoa vibali vya
ajira mpya katika mwaka wa fedha 2026/27 kwa sekta ya afya pamoja na
kada nyingine, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza uhaba wa
madaktari na wauguzi nchini.
Akizungumza
Mei 12, 2026 katika Kongamano la Kwanza la Kisayansi la Wauguzi
lililoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika
katika Hotel Verde Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi alisema Serikali
itaendelea kuwekeza zaidi katika kuboresha huduma za afya ili
kuhakikisha wananchi wanapata matibabu bora na ya kisasa.
Alieleza
kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya
ikiwemo ujenzi wa Hospitali Mpya ya Mnazi Mmoja pamoja na Hospitali ya
Saratani Binguni, sambamba na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa na
kuimarisha mafunzo kwa watumishi wa sekta hiyo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...