Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026. Katika mazungumzo yao Mhe. Rais Dkt. Samia amemuomba Nyota huyo Ivory Coast kuwa Balozi wa Tanzania kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Aidha, Rais Dkt. Samia ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na mchezaji huyo kubadilishana uzoefu wa kuendesha Vituo vya michezo nchini (Sports Academy). Mchezaji huyo amemshukuru Rais Dkt. Samia na kuonesha utayari wa kushirikiana na Serikali. Pamoja na mafanikio kadhaa aliyoyapata katika Mpira wa miguu, Mwaka 2005, alifanya ushawishi uliosaidia kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao vilivyodumu kwa miaka kadhaa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...