
Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Rais
wa Kenya, William Ruto, amempongeza Jaji Mohammed Abdullahi Warsame
baada ya kuapishwa rasmi kuwa jaji wa 14 wa Mahakama ya Juu ya Kenya,
akieleza kuwa uzoefu wake mkubwa utasaidia kuimarisha utoaji wa haki
nchini humo.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika Ikulu ya
Nairobi, Rais Ruto alisema ana imani kuwa Jaji Warsame ataleta mchango
chanya katika mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Kenya kupitia weledi na
uzoefu wake wa muda mrefu katika sekta ya sheria.
“Unaungwa mkono kikamilifu na tunakuombea mafanikio unapoanza jukumu
hili muhimu la kulitumikia taifa letu,” alisema Ruto wakati wa hafla ya
kuapishwa kwa jaji huyo.Katika hafla hiyo pia, Rais Ruto
aliwapongeza Evans Thiga Gaturu na Jedidah Wakonyo Waruhiu baada ya
kutunukiwa hadhi ya Senior Counsel, akisema wameonyesha mchango mkubwa
katika kuimarisha utawala wa sheria na demokrasia ya kikatiba nchini
Kenya.
Ruto
alisema Serikali ya Kenya itaendelea kushirikiana na mihimili mingine
ya dola kuhakikisha haki inatendeka na mfumo wa sheria unaendelea
kuimarika kwa manufaa ya wananchi wote.
Hafla hiyo ilihudhuriwa
pia na Naibu Rais wa Kenya, Kithure Kindiki pamoja na Jaji Mkuu na Rais
wa Mahakama ya Juu Kenya, Martha Koome.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...