Mbunge wa Viti Maalum, Nasriya Nasir Ali ameishauri Serikali kuhakikisha lugha ya alama inaingizwa rasmi kama somo katika ngazi zote za elimu ili kuongeza usawa na ujumuishaji kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia nchini.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bungeni jijini Dodoma, Mei 8, 2026, Nasriya ameipongeza Wizara hiyo kwa kuendelea kuboresha mifumo ya elimu inayolenga kutoa fursa sawa kwa makundi yote, hususan watu wenye ulemavu.
Amesema kufundishwa kwa lugha ya alama kwa upana kutasaidia kuboresha mawasiliano kati ya wanafunzi na walimu, na hivyo kuongeza ushiriki wa watu wenye ulemavu wa kusikia katika masomo na shughuli mbalimbali za kijamii.
Aidha, ameongeza kuwa hatua hiyo itakuwa chachu ya kuimarisha elimu jumuishi nchini, kwa kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma kutokana na changamoto za mawasiliano.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...