Na Pamela Mollel,Arusha 

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Urusi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uchimbaji na uchakataji wa madini pamoja na uwekezaji katika viwanda vikubwa vya dawa vitakavyosaidia kuboresha huduma za afya na kuongeza ajira kwa wananchi

Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akizungumza katika jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililowakutanisha viongozi, wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa hayo mawili

“Tanzania itaendelea kufungua milango ya uwekezaji na kushirikiana na mataifa mbalimbali ili kuhakikisha sekta muhimu za uzalishaji zinakuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi,” amesema Profesa Kitila Mkumbo

Amesema ushirikiano huo utafungua fursa mpya za maendeleo, kuongeza thamani ya mazao na madini pamoja na kusaidia upatikanaji wa teknolojia na huduma muhimu kwa wananchi

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi, Maksim Reshetnikov amesema Tanzania ni moja ya nchi zenye fursa kubwa za uwekezaji kutokana na mazingira mazuri ya biashara yanayoendelea kuimarishwa

“Urusi ipo tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali za uchumi kwa manufaa ya mataifa yote mawili,” amesema Maksim Reshetnikov

Jukwaa hilo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi limewakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji pamoja na viongozi mbalimbali kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji, kujadili changamoto za biashara na kupanua masoko kati ya nchi hizo mbili.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...