Na Byera Deus,Kagera
SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya kilimo(TADB) imeendelea na utoaji wa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba ili kuwezesha vijana wengi kujiajili kupitia uvuvi.
Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa kukabidhi mitaji ya kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyobuniwa na Vijana wa (Build Better Tomorrow (BBT)-Uvuvi Mkoa wa Kagera katika mwalo wa -Bilolo Kemondo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara hiyo Emelda Adam amesema programu hiyo inalenga kupambana na changamoto ya ajira kwa vijana na kuongeza nguvu ya vijana kujitegemea
Amesema vijana walionufaika na vizimba mkoani Kagera walipata mafunzo ya ukuzaji wa viumbe hai mwaka 2024 na wametoka mikoa mbalimbali wakiwa wameiva kwa ujuzi wa uendeaji wa vizimba hivyo ambapo wataanza kuvuna Samaki baada ya miezi 7.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa programu ya “BBT” Kanda ya Ziwa Peter Masumbuko amesema vijana 47 wa Mkoa wa Kagera wamenufaika na programu hiyo.Shilingi bilioni saba zimetengwa kwa ajili ya vijana zaidi ya 300 wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Ameongeza kwa Kanda ya ziwa Program ya kuwanuia vijana mpaka kujiajiri inatekezwa mikoa ya Kagera,Mwanza ,Geita na Mara na vijana hao wote wameisha hitimu mafunzo yao
Amefafanua kwa kuanzia Kila kijana anapata kuzimba kimoja japo wanawaweka katika makundi na mradi unakuwa na Nyumba ya mlinzi Boti ya ufatiliaji na Camera ya Kuona Nini kinaendelea katika mradi huo ambao serikali itawalea vijana kwa miaka minne Hadi wajikimu
Awali Mkuu wa Wilaya Erasto Sima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ramadhan Kido amesema ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya programu hiyo na kuwaasa vijana wanufaika wa mkopo huo kuutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Amesema baada ya ufunguzi wa vizimba mvuvi yeyote atakayekamatwa katika eneo hilo atachukuliwa kama mvuvi haramu kwani sehemu hiyo haipaswi kusogelewa badala yake inatakiwa kulindwa Kwa nguvu zote ili kuleta matokeo Chanya .
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Sadothi Ijunga ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuukumbuka mkoa wa Kagera huku akitoa rai kwa vijana kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha walizozipata.
Katika hatua nyingine baadhi ya wanafuika akiwemo Marius Pius amesema mafunzo waliyopatiwa yamehusisha vijana wa aina zote na wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa kutimiza ahadi yake kwa vijana hao.
“Tulikuwa tayari tuko mtaani baada ya mafunzo lakini leo jambo limetimia ,hivyo sisi kama vijana lazima tusimame imara na tulete matokea chanya ambayo pia yatasaidia vijana wengine kujiajili.Tuko tayari kulinda vizimba hivi na kuzalisha kwa weledi,”amesema Pius.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...