Na Mwandishi Wetu.

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wameshiriki katika semina kuhusu Mpango Mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa,Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma  Waziri katika mada yake amesema Gridi ya  Maji ya Taifa ni mfumo wa kimkakati wa usambazaji maji kutoka kwenye vyanzo vya uhakika na kuyapeleka katika maeneo yenye uhaba wa maji nchini.

Ameongeza hadi sasa  Wizara ya Maji imekamilisha vipande vya  mtandao wa Taifa wa maji ikiwamo kutoa maji ziwa Victoria kwenda mikoa ya Shinyanga, Tabora na Shelui katika mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Waziri wa Maji  Jumaa Aweso akihitimisha mada amewaomba ushirikishwaji  wa jamii na  ushirikiano kwa wabunge wote ili kuhakikisha mpango mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa unafanikiwa ili kuhakikisha wananchi wote  wanapata huduma ya majisafi na salama na kuchochea ukuaji wa uchumi ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2050).









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...