Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameongoza mamia ya wafanyakazi Mkoani humo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Mnazi mmoja na kuwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na maarifa huku wakifanya tathmini ya matokeo ya mafanikio au tija ya utendaji wao kwenye taasisi wanazozifanyia kazi

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo RC Chalamila amewataka wafanyakazi kutumia nguvu na maarifa yao vizuri kwenye kutekeleza wajibu wao wawapo kazini lakini pia kila mfanyakazi kutafakari mchango wake kwenye taasisi au mamlaka anayoifanyia kazi ili wanapopaza sauti zao kwa ajili ua stahiki zao utendaji wao pia uwe na tija kwenye taasisi zao

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwapongeza waajiri wa sekta binafsi kwa kuisaidia Serikali kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira huku akiwataka kifuata taratibu, kanuni na sheria za kazi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na ameweka msisitizo kwa wafanyakazi kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi

Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amewapongeza wafanyakazi Mkoani humo kwa kazi nzuri wanazozifanya huku akiendelea na msimamo wake wa kuzitaka taasisi kutoa zawadi ya pesa taslimu hadharani kwa watumishi waliofanya vyema kwenye utumishi wao

Akisoma risala ya wafanyakazi Mkoani humo kwa niaba ya katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam, Katibu wa Chama cha Walimu Mkoani humo Abraham Kamwela ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha mazingira, haki na maslahi kwa wafanyakazi huku akiiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo kupunguza mfumuko wa bei, kupunguza msongamano wa magari, kuwezesha uwepp wa nyumba za gharama nafuu lwa wafanuakazina kuendelea kuboresha vipato vya wafanyakazi hasa ikizingatiwa changamoto ya ongezeko la gharama za maisha kwa kila nyanja

Maadhimosho hayo ya Mei Mosi yamebeba kaulimbiu isemayo "Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050"










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...