▪️Wajadili mipango endelevu ya ujenzi wa miundombinu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya kikao kazi na wabunge wa mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha.

Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili maendeleo ya miradi ya kimkakati ya miundombinu katika mikoa hiyo hususan ukamilishaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza pamoja na viwanja vya ndege vya Serengeti na Musoma.

Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Spika, Bungeni jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 15, 2026, pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wakuu wa taasisi za usafirishaji na miundombinu ikiwemo reli, barabara na viwanja vya ndege pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...