Zaidi ya wananchi 54,000 wamenufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea mkoani Dodoma katika kipindi cha siku tatu za awali tangu kuanza kwake Mei 1, 2026.

Akizungumza leo Jumatatu, Mei 04, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu wa Msaada wa Kisheria, Bi. Lucy Darabe Diganyeck, amesema kuwa kampeni hiyo ya awamu ya pili inatekelezwa katika halmashauri zote za mkoa huo kwa muda wa siku 15 hadi Mei 15, 2026.

Ameeleza kuwa kampeni hiyo inalenga kutoa elimu ya kisheria, ushauri wa kisheria pamoja na kusaidia uandishi wa nyaraka mbalimbali za kisheria kwa wananchi, na inahusisha usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala ikiwemo ya ardhi, ndoa na masuala mengine ya kisheria.

Kwa mujibu wa takwimu za wananchi waliopata huduma,  wanaume ni takribani 25,000 huku wanawake wakiwa zaidi ya 28,000, wengi wao wakiwa wanafunzi, madereva wa bodaboda, wafanyabiashara ndogondogo pamoja na makundi mengine ya kijamii.

Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma, hasa wenye changamoto za migogoro ya ardhi na masuala mengine ya kisheria, kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zinazotolewa bure na serikali.

Baadhi ya wananchi waliofikiwa na huduma hiyo wameeleza kufurahishwa na kampeni hiyo, wakisema inatoa matumaini ya kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zao za kisheria kutokana na maandalizi mazuri na huduma bora wanazozipata.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...