
Na Mwandishi Wetu
NDOTO za vijana wa Tanzania wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi kwa mwaka wa masomo 2026/2027 zimeingia hatua muhimu baada ya Global Education Link kuwakutanisha wanafunzi hao pamoja na wazazi na walezi wao kwa ajili ya kuhakiki nyaraka na kukamilisha maandalizi ya safari.
Kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya Global Education Link, Dar es Salaam, kililenga kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na nyaraka sahihi, taarifa za kutosha na maandalizi muhimu kabla ya kuondoka nchini kwenda kuanza masomo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, alisema lengo kuu la kikao hicho ni kuhakiki na kukamilisha nyaraka muhimu za wanafunzi, kujibu maswali ya wazazi na kuhakikisha changamoto zinazoweza kuchelewesha safari zinapatiwa ufumbuzi mapema.
Mollel alisema wazazi na walezi wanapaswa kujiridhisha kuhusu utambuzi wa kisheria wa chuo kilichochaguliwa kwa kupata uthibitisho rasmi kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, ili kuhakikisha sifa zitakazopatikana baada ya kuhitimu zinatambuliwa na mamlaka husika nchini.
Kwa mujibu wa Mollel, safari ya masomo nje ya nchi haiishii katika kupata nafasi ya kujiunga na chuo pekee, bali inahitaji maandalizi kuhusu visa, malazi, usafiri, usalama, sheria, utamaduni wa nchi husika na uwezo wa mwanafunzi kuishi kwa nidhamu na uwajibikaji.
Kwa upande wao, wazazi na walezi walioshiriki kikao hicho walisema wameridhishwa na namna Global Education Link ilivyowahudumia na kuwapatia majibu kuhusu hatua mbalimbali za udahili na maandalizi ya safari.
Mmoja wa walezi hao, Asuba Omary kutoka Zanzibar, alisema kikao hicho kimemsaidia kufahamu mambo ya kuzingatia kabla ya mzazi kuamua kumsomesha mtoto katika chuo kikuu cha nje ya Tanzania.


.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...