Taasisi ya INADES Formation Tanzania imeadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti 200 ya kivuli na matunda katika Shule ya Sekondari Kisima cha Ndege iliyopo Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Zoezi hilo ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya “Panda Mti Tuilinde Kesho” iliyozinduliwa Januari 2026, yenye lengo la kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha utunzaji wa mazingira.

Akizungumza baada ya shughuli ya upandaji miti iliyofanyika Juni 5, 2026, Mwakilishi wa INADES Formation Tanzania, Paul Ephras Chugu, amesema taasisi hiyo imefanikiwa kupanda miti zaidi ya 15,000 katika vijiji vinne vya Wilaya ya Bahi tangu kuanza kwa kampeni hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Joyce Anania Jackson, ameipongeza INADES Formation Tanzania kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya taasisi hiyo na halmashauri katika kutekeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisima cha Ndege,  Mwalimu wa Mazingira na Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira wa shule hiyo, wamepongeza juhudi za taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Mazingira Duniani yaliambatana na bonanza la michezo lililowakutanisha wanafunzi wa shule hiyo, wanafunzi kutoka shule jirani pamoja na wananchi wa vijiji vya jirani, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...