Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb) afungua kikao cha majadiliano kuhusu DPI for Inclusive Growth katika Wiki ya Kimataifa ya Teknolojia Huria (UN Open Source Week 2026) jijini New York, Marekani.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoandaa maadhimisho hayo yanayohudhuriwa na mataifa na wadau mbalimbali wa teknolojia ulimwenguni.
Katika hotuba yake ya ufunguzi Waziri Kairuki alisema Tanzania imepiga hatua katika ujenzi wa mifumo ya kidijitali ikiwemo utambuzi wa kidijitali, mifumo ya malipo na mifumo ya kubadilishana taarifa kati ya sekta mbalimbali, ambayo ni msingi wa mageuzi ya kidijitali na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Waziri Kairuki amesema Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha miundombinu ya kidijitali kupitia Mkongo wa Taifa wenye zaidi ya kilomita 27,000 za nyuzi za mawasiliano, vituo vya kuhifadhi data na mifumo inayounganisha taasisi za umma na binafsi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika matumizi ya teknolojia huria ili kuimarisha ubadilishanaji wa taarifa, usalama wa mtandao na matumizi salama ya Akili Unde (AI), akieleza kuwa hakuna nchi wala mwananchi anayepaswa kuachwa nyuma katika safari ya uchumi wa kidijitali.
.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...