Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, ambao unatekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, umepanga kuwawezesha wanawake na vijana 6000 ndani ya muda wake wa utekelezaji wa Miaka Mitano wa Mradi huo, ambao ukiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika ujasiliamali wa Biashara ya Mifugo.

Akizungumza leo Juni 1, 2026 Mkoani Morogoro, katika Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu hiyo ya BBT, Meneja Mradi wa BBT Upande wa Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii, Bi. Neema Urassa amesema Mradi huo una lengo la kuwawezesha Wanawake na Vijana kupitia shughuli za unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo kibiashara pamoja na Kilimo cha Malisho ya Mifugo.

"Mradi huu unawalenga zaidi Wanawake na vijana, ambao kupitia Mradi huu watapata kujifunza vitu mbalimbali kwa vitendo katika mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya mifugo, hususan mbuzi na Kondoo na Kilimo cha Malisho ya Mifugo, ili baadae wawe na uwezo wa kuingia kwenye biashara za unenepeshaji wa mifugo kwa lengo la kujiongezea kipato pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa." Amesema Bi. Urassa

Aidha, Bi. Urassa amesema baada ya vijana kupata ujuzi huo, matarajio ya Serikali ni kuwa vijana wataweza kujiajiri wenyewe, kuanzisha biashara zao, na kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto ya ajira nchini, ambapo vijana watakaonufaika watakuwa na fursa ya kupatiwa mikopo isiyo na dhamana kwa ajili ya kuendeleza biashara zao baada ya mafunzo.

Vilevile, Bi. Urassa,  ameweka wazi kuwa Mradi huo unatokana na Uongozi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kwa kina changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, ndiyo maana Mheshimiwa Rais amechukua juhudi za makusudi kuhakikisha fedha hizo zinapatikana kwa ajili ya kuboresha maisha ya vijana kupitia miradi yenye tija kama huo wa BBT ambao unaendana na Dira ya Taifa ya Mwaka 2050.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...