MANYARA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi mkuu wa Chama chao ni kusikiliza wananchi na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi.
Kihongosi amesema hayo leo Juni Mosi, 2026 wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa Shina Namba Moja, Tawi la Masakta, Kata ya Masakta wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Kanda ya Kaskazini.
Amesema CCM imeendelea kuwa karibu na wananchi kwa sababu imejengwa katika misingi ya kusikiliza maoni yao, kutambua mahitaji yao na kuyafikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
“Kazi hizi zinafanywa na chama kwa sababu chama hiki ndicho kinaunda Serikali. Lakini msingi wa CCM ni kusikiliza watu, kutatua shida za watu na zile changamoto ambazo zinakuwa kubwa basi zipelekwe katika maeneo husika ili zipatiwe ufumbuzi,” amesema Kihongosi.
Katika hatua nyingine, Kihongosi amesema chama kitaendelea kufuatilia suala la kupandisha hadhi zahanati ya Masakta na kuwa kituo cha afya kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
“Kama vigezo vitakuwa vimekidhi, niwahakikishie chama kitaendelea kusimamia kwa asilimia mia moja. Sote kwa pamoja tutashirikiana kuhakikisha jambo hili linapatiwa ufumbuzi wake,” amesema.
Kihongosi ameeleza hayo akujibu ombi la wananchi wa Kata hiyo ambalo lilihusu kupandishwa kwa hadhi ya Zahanati yao ya Kijiji kuwa Kituo cha Afya kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohudumiwa katika zahanati hiyo na kuomba kuongeweza madaktari.
Awali akiwasilisha taarifa ya shina, Katibu wa Shina Namba Moja, Dismas Gwasima, aliiomba CCM na Serikali kuangalia uwezekano wa kupandisha hadhi zahanati ya Masakta na kuwa kituo cha afya kutokana na ongezeko la idadi ya wananchi wanaohudumiwa na kituo hicho.
Alisema zahanati hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa zaidi ya miaka 20, lakini kwa sasa mahitaji ya huduma za afya yameongezeka sambamba na kukua kwa idadi ya watu, hali inayosababisha wananchi kukosa baadhi ya huduma muhimu zinazopatikana katika vituo vya afya.
Gwasima alisema wananchi wanahitaji kuongezewa huduma za mama na mtoto, huduma za upasuaji, watumishi wa afya pamoja na nyumba za watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma katika eneo hilo.





.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...