Na Victor Masangu,Kibaha
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amewahimiza wanawake kuweka misingi imara ya kutumia fursa za mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Hamashauri kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Vullu ameyabainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo ameweza kutembelea katiika kata mbili za Tumbi pamoja na Kata ya Kongowe ambapo ameambatana na kamati ya utekelezaji ya Mkoa pamoja na vingozi ngazi ya Wilaya.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo ameweza kupata fursa ya kutembelea baadhi ya miradi ikiwemo katika sekta ya elimu ambapo ameweza kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa choo salama katika wa sekondari ya Kibaha pamoja na kituo cha afya Kongowe.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwa ajili ya kuwashukuru umoja wa wanawake UWT kwa kuweza kuwa pamoja na mshikamano wa kukiwezesha chama cha mapinduzi kuweza kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwapoitisha viongozi katika ngazi mbali mbali ikiwemo udiwani, Ubunge pamoja na nafasi ya Urais.
Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjni Cesilian Ndaru amesema kwamba lengo lako kubwa ni kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya kuwa na vitega uchumi ambavyo vutaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kijikwamua kiuchumi.
Katibu Ndaru amebainisha kwamba umoja huo wameweka mipango madhubuti ya kuwa na miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuanzisha miradii ya kuwa na nyumba za makatibu kila kata kwa ajili ya kuwawezesha makatibu kuwa na sehemu na makazi ya kusihi ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Naye mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Mama Selina Koka ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini amesema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wanawake katika kuhakikisha kwamba wanaimarisha jumuiya hiyo.
Mama Koka amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana kwa pamoja na viongozi wenzake katika kufanya kazi kwa bidii na kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta chanchu ya maendfeleo ikiwa pamoja na kuwainua kiuchumi wanawake wenzake.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani imefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo ameweza kupata fursa ya kutembnelea baadhi ya mikradi ya maendeleo ikiwemo katika shule ya sekondari ya wasichana Kibaha pamoja na kituo cha afya Kongowe ikiwa pamoja na kuzungumza na wanawake wa umoja huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...