Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wazazi na walezi mkoani Geita wametakiwa kuthamini na kulinda haki za watoto kwa kuwakinga dhidi ya ukatili na unyanyapaa.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Maadhimisho hayo ya kimkoa yamefanyika katika Kata ya Nyawilimilwa, Wilaya ya Geita.
Mhe. Komba amesema Serikali haitaona aibu kuwachukulia hatua za kisheria wazazi au walezi wanaowanyima watoto wao haki ya msingi ya kupata elimu na haki nyingine zilizowekwa na sheria za nchi. Amesema ulinzi wa mtoto ni wajibu wa kila mzazi na jamii kwa ujumla.
Akitoa taarifa ya utekelezaji, Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Geita, Bw. Frank Moshi, ameeleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na mikakati inayoendelea kutekelezwa ili kudhibiti vitendo vya ukatili na uhalifu unaofanywa dhidi ya watoto mkoani humo. Amesema jitihada hizo zimeleta matumaini kwa watoto wengi waliokuwa katika mazingira hatarishi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la NELICO linalojihusisha na utetezi na ulinzi wa haki za watoto mkoani Geita, Bi. Paulina Alex Majogoro, amesema shirika hilo linaendelea kutoa msaada kwa watoto. Msaada huo ni pamoja na ushauri wa kisheria, sare za shule na mahitaji mengine muhimu kwa familia zenye kipato duni.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya kuhimiza jamii kutoa kipaumbele kwa ustawi na usalama wa mtoto ili kujenga taifa lenye vizazi vijavyo vyenye maadili na elimu.



.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...