Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Vedastina Kagombora amesema kuwa Suala la ujumuishaji sio jukumu la Sekta moja bali ni la kila Wizara kushirikiana ili kuweka mazingira rafiki katika upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo afya,Elimu na Miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Vedastina ameyasema hayo Jijini Dodoma katika kikao kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu na Wawakilishi wa Madawati ya wenye ulemavu wa Wizara zote na baadhi ya Taasisi za Serikali.
Ambapo amesema kuwa umuhimu wa madawati haya ya kuleta haki,ushiriki wa watu wenye ulemavu yanayojumuisha katika mipango na Sera,Bajeti,Programu na shughuli zote za maendeleo ni za Wizara husika na sio kuyaacha yashughulikiwe na Ofisi inayoratibu masuala ya watu wenye ulemavu pekee.
"Ni muhimu kutambua kuwa ujumuishaji sio jukumu la Sekta au Wizara moja pekee bali ni wajibu na jukumu la kila Wizara na sisi wote kuendelea kushirikiana katika kuweka mazingira rafiki yanayowezesha upatikanaji wa huduma zote muhimu ikiwemo Elimu jumuishi,Huduma za Afya,Ajira,Teknolojia Saidizi,Huduma za Kijamii,Miundombinu Fikivu pamoja na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika kutoa maamuzi yanayoweza kuwafikia watu weny Ulemavu".
Aidha Vedastina amebainisha mafanikio makubwa waliyoyapata katika kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu kuwa pamoja na mapitio ya Sera ya watu wenye ulemavu,kuunda madawati ya watu wenye ulemavu katika Wizara mbalimbali,kupata mikopo ya Serikali na pia kutengeneza mfumo wa taarifa za watu wenye ulemavu ambapo wanasajiliwa na kupata namba ya usajili ili kuwatambua kwa urahisi mahali walipo.
Kwa upande wake Mdoka Omary ambaye ni Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi wa Taifa ya Takwimu ameeleza kuwa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliendelea kutumia maswali sita kulingana na Mwongozo wa Kimataifa wa Washington Group pamoja na nyongeza ya maswali mengine ya ulemavu kutoka SHIVYAWATA ambapo Maswali yaliyoulizwa kwenye sehemu ya hali ya ulemavu, ni Ualbino, Kuona, Kusikia, Kutembea/kupanda ngazi, Kukumbuka/kufanya vitu kwa umakini, Kujihudumia, Kuwasiliana na “Aina Nyingine ya Ulemavu” ambapo Aina nyingine ya ulemavu ilijumuisha maswali ya ulemavu wa Mdomo Sungura, Kichwa Kikubwa, Mgongo Wazi; Kuumia Uti wa Mgongo; Kifafa; Mabakamabaka ya Ngozi, Mbalanga (Storiasis); Usonji (Autism); Matatizo ya Afya ya Akili; Ulemavu wa Akili; Mtu Mwenye Kimo Kifupi; Ukoma na mtu Mwenye Kibiongo.
Aidha, kwa mara ya kwanza waliuliza maswali yanayohusu chanzo cha ulemavu na iwapo mtu mwenye ulemavu anatumia kifaa saidizi, na Kwa mujibu wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka huo wa 2022, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na watu wenye ulemavu 5,347,397,na kiwango cha ulemavu nchini kiliongezeka kutoka asilimia 9.3 mwaka 2012 hadi asilimia 11.2 mwaka 2022.
Naye Harun Harun ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI,amesema kuwa Ofisi hiyo kupitia sektretarieti za Mikoa na Halmashauri kuna Mikakati ambayo inafanyika ya kuwabaini watu wenye ulemavu wa kila aina na pia kutenga bajeti kwa makundi haya ambapo bajeti imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Ambapo pia Ofisi hiyo imekuwa na kamati katika ngazi za Halmashauri za watu wenye ulemavu ambazo zimeundwa kwenye Mikoa yote 26 Halmashauri 184 na kata zaidi ya 3,400 ili kubaini na kutambua changamoto wanazokutana nazo watu hawa wenye ulemavu ili Maafisa Ustawi waweze kuwafikia kwa urahisi.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu ilikondoisha huduma za watu wenye ulemavu katika ngazi za Wizara kwa kuunda madawati ya watu wenye ulemavu mnamo mwaka 2018
Imewakutanisha Wawakilishi hao ili kuwajengea uelewa na kuwakumbusha juu majukumu yao kwa madawati hayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...