📍 Chinangali Park, Dodoma
TAWIRI imeendelea kutoa elimu kwa wadau wakiwepo wananchi ambapo wakulima wamepata elimu ya umuhimu wa wadudu katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori sambamba na mchango wa wadudu katika kilimo ikiwa ni pamoja na uchavushaji.
Vilevile wananchi wamepata uelewa juu ya juhudi zinazofanywa na TAWIRI chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii za kuwahifadhi wanyamapori kwa kutumia taarifa sahihi za kisayansi.
“tunashukuru kwa elimu nzuri, kabla ya elimu hii nilijua wanyamapori wanakaa porini wanajihudumia lakini leo nimepata uelewa wanyamapori wanatibiwa, wanahesabiwa, wanafuatiliwa mienendo yao kwa kutumia teknolojia”
amesema Enderesa Salla miongoni mwa wananchi waliotembelea banda la TAWIRI
TAWIRI tunawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kuja kupata elimu ya sayansi ya wanyamapori kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza Utalii.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...