Kamati ya Wataalam ya Serikali ya Maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) imeweka mkazo katika kuhakikisha miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara inayotekelezwa kuelekea michuano hiyo inakamilika kwa wakati, ili kuboresha usafiri na usafirishaji.


Akifungua kikao kazi cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini Arusha tarehe 26 Juni, 2026, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Mkombachepa, amesema, Mkoa wa Arusha unaendelea kushuhudia utekelezaji wa miradi mingi ya barabara katika maeneo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya AFCON 2027.

 Amesisitiza Kamati hiyo kujadili kwa kina na kuweka mikakati madhubuti ya kufuatilia utekelezaji na ukamilishaji wa miradi hiyo, hususan katika maeneo na vituo vitakavyotumika wakati wa mashindano.

Awali, Mkurugenzi wa  Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Boniface Tamba, amesema Kamati hiyo ina jukumu la kuratibu, kufuatilia na kuhakikisha utekelezaji wa miradi yote ya maandalizi ya AFCON 2027 inafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.

Kamati hiyo, inaundwa na wajumbe kutoka wizara na taasisi mbalimbali za Serikali,ikiwa na lengo la kuimarisha uratibu wa maandalizi na kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kuandaa kwa mafanikio michuano hiyo mikubwa Afrika.









 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...