MOSHI.
VIJANA wameaswa kutokukubali kurubuniwa, kushawishiwa wala kutumika kwa namna yoyote ili kuhatarisha Amani mshikamano na umoja wa Taifa kwa maslahi binafsi ya watu au makundi yenye nia zisizo njema kwa nchi.
Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Ivan Moshi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Kilimanjaro kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa.
Akisoma tamko hilo, Moshi alisema kuwa, wanatambua athari kubwa zinazoweza kusababishwa na migogoro, vurugu na mipasuko ya kijamii katika Uchumi na ustawi wa wananchi na kutoa wito kwa vijana kuendelea kuzipuuza kauli, vitendo na propaganda zinazolenga kuleta taharuki, migawanyiko au kuvuruga amani.
“Baraza la UVCCM mkoa wa Kilimanjaro linawapongeza vijana wa Kilimanjaro na Tanzania kwa kuendelea kuonyesha uzalendo, uvumilivu, busara na mshikamano katika kuilinda amani na utulivu wa Taifa letu, tunatambua amani ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa” alisema Ivan.


.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...