Na Mwandishi Wetu, Uswisi
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Jijini Geneva, nchini Uswisi.
Akizungumza leo Juni 4, 2026 Waziri Sangu amesema mkutano huo umekuwa na manufaa makubwa kwa Taifa katika kujadili masuala ya haki za wafanyakazi, kusimamia viwango vya kazi ili kuwa na stahiki kulingana na makubaliano ya pamoja chini ya Shirika la Kazi Duniani.
Amebainisha maeneo makuu ya mjadala katika mkutano huo wa mwaka 2026 ni Masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Kazi Duniani, Utekelezaji wa mikataba mbalimbali ambayo Tanzania imeridhia chini ya ILO na Matumizi ya Akili Unde (AI) inavyoweza kutumika katika kuhakikisha kazi za staha zinazingatiwa kwa wafanyakazi.
Pia amesema kuwa katika mkutano huo wameweza kujadili na Wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) kutoka Tanzania Bara na Visiwani ili kuona namna bora ya kushirikiana na kuwa na majadiliano ya kijamii ambayo yanaleta tija hususan katika nyakati hizi za matumizi ya teknolojia na ukuaji wa uchumi wa kidijitali.
Wakati huo huo Waziri Sangu amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu wadau wa utatu kushiriki katika mkutano huo ambao unawawezesha kubadilishana uzoefu na kujadili masuala yanayohusu ustawi wa sekta ya kazi.
Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Jijini Geneva, nchini Uswisi unashirikisha wawakilishi wa Serikali, Waajiri na Wafanyakazi kutoka nchi wanachama 187. Mkutano huo ulianza rasmi tarehe 1 Juni, 2026 na utahitimishwa Juni 12, 2026.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...