"....Mimi nikifa nitaaga siwezi kuondoka kimya kimya", Seif Kisauji amemwambia Ankal kwa utani wakati Mwanamuziki huyo maarufu kama Babu wa TikTok, akikanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa amefariki dunia.

Babu wa TikTok akiongea akiwa msikiti wa Maamur ulioko Upanga jijini Dar amekanusha taarifa hizo na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa yuko hai na anaendelea vizuri.

Ameeleza kuwa chanzo cha mkanganyiko huo ni kifo cha mtoto wa familia yao, Mabrouk Kisauji, na si yeye, na kwamba wapo hapo Maamur kukamilisha mipango ya safari ya Tanga, na kwamba yeye na familia yake wanasafiri kuelekea huko leo kwa ajili ya kuhudhuria mazishi.

Kisauji kaongea haya yote baada ya kuona video yake akiimba kusambazwa mitandaoni ikiwa imeambatanishwa na madai ya uongo kwamba amefariki, jambo lililozua taharuki miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Amewasihi watumiaji wa mitandao kuwa makini na taarifa za upande mmoja kwani katika zama hizi za kila mtu kujifanya mwandishi wa habari, taarifa zisizo sahihi ni nyingi mno.

Pia amewataka walio wanahabari wasiwe na papara za kuchapisha taarifa ammbazo hazijathibitishwa kwa kuwa hiyo inawavunjia heshima kwa kuonekana ni waongo na wadaku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...