Na Janeth Raphael - MichuziTv
Serikali imezindua Mradi wa Twiga Future Forward Education Program, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Barrick Tanzania, ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini na kuongeza fursa za wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora.
Akizindua mradi huo leo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa, wilayani Kongwa mkoani Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwa nguvu katika sekta ya elimu kwa kuwa ndiyo msingi wa kujenga uchumi wenye ushindani na maendeleo endelevu ya Taifa.
Amesema uwekezaji katika elimu unalenga kuandaa rasilimali watu yenye maarifa, ujuzi na maadili, ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kuongeza tija katika uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.
"Elimu bora haiwezi kupatikana bila kuwa na mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia. Ndiyo maana Serikali inaendelea kuwekeza katika ujenzi wa madarasa, mabweni na miundombinu mingine muhimu ili kila mtoto wa Kitanzania aweze kufikia ndoto zake," amesema Prof. Shemdoe.
Prof. Shemdoe amesema kupitia ushirikiano kati ya Serikali na Barrick Twiga Minerals, zaidi ya Shilingi bilioni 70 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini, ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo.
Ameeleza kuwa mafanikio ya mradi huo yametokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, yaliyozaa makubaliano ya kampuni hiyo kutoa msaada wa Dola za Marekani milioni 30 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.
Katika kuhakikisha mradi unaleta matokeo yaliyokusudiwa, Prof. Shemdoe amemuelekeza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha fedha zilizobaki zinatumika kujenga bwalo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa jengo hilo muhimu.
Aidha, ameitaka timu ya Serikali inayoshughulikia majadiliano na Barrick kurejea mezani kujadili uwezekano wa kupata ufadhili mwingine wa Dola milioni 30 au zaidi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, ikiwa ni maandalizi ya ongezeko kubwa la wanafunzi litakalotokana na madarasa mawili ya elimu ya msingi kuhitimu kwa wakati mmoja mwaka 2028.
Pia amezitaka halmashauri zote zinazotekeleza mradi huo kuhakikisha zinasimamia kikamilifu utekelezaji wake, huku wakandarasi wakitakiwa kuzingatia viwango vya ubora na kuhakikisha miundombinu inayojengwa inadumu kwa muda mrefu kupitia matengenezo ya mara kwa mara.
Vilevile, amewataka wakuu wa shule, walimu, wazazi na wananchi kushiriki katika kulinda miundombinu hiyo ili iendelee kunufaisha wanafunzi wa sasa na vizazi vijavyo.
Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa awamu ya pili ya mradi inapaswa kukamilika ifikapo Agosti 30 mwaka huu, ili kutoa nafasi ya kuanza kwa awamu ya tatu kwa wakati.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, amesema kampuni imepokea maelekezo ya Serikali kuhusu mahitaji ya ziada ya miundombinu kwa ajili ya wanafunzi watakaomaliza elimu ya msingi mwaka 2028 na kwamba itayafanyia kazi kupitia kamati inayoratibu utekelezaji wa mradi huo.
Ngido amesema hadi sasa Barrick tayari imetumia Dola za Marekani milioni 20, huku Dola milioni 10 zilizobaki zikitarajiwa kuelekezwa katika maeneo yatakayokubaliwa kwa pamoja na Serikali kulingana na mahitaji yaliyopo.
Kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo, utakapokamilika utajumuisha ujenzi wa madarasa 1,090 yatakayohudumia wanafunzi 54,500, mabweni 270 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 21,600, pamoja na matundu ya vyoo 1,640 yatakayowanufaisha wanafunzi 49,200 katika halmashauri zote za Tanzania Bara.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Atupele Mwambene, amesema mradi huo unalenga kuongeza uwezo wa shule za sekondari kupokea wanafunzi wengi zaidi, kupunguza msongamano madarasani, kuongeza nafasi za kuendelea na elimu ya juu ya sekondari pamoja na kuinua kiwango cha ufaulu nchini.
Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika miradi ya maendeleo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa katika elimu unaleta matokeo chanya kwa Taifa na kizazi kijacho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...